![]() |
Ulimwengu, mfungaji wa bao la Ngorongoro |
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa
miaka 20, Ngorongoro Heroes imefanikiwa kusonga mbele katika kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika usiku huu, baada ya kutioa Sudan kwa jumla ya mabao
4-3.
Ngorongoro leo imekubali kichapo chepesi
cha mabao 2-1 ugenini, kwenye Uwanja wa Khartoum, baada ya awali kushinda 3-1 Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam wiki mbili zilizopita na sasa itachuana na Nigeria
Raundi ya Pili, mechi ya kwanza ikicheza Julai 28, mwaka huu Dar es Salaam.
Sudan walipata mabao yao kupitia kwa Mohammed
Abdelrahman dakika ya 10 na Ahmad Nasr kwa penalti dakika ya 65, wakati bao la
Ngorongoro lilifungwa na mshambuliaji wa Tout Puissant Mazembe ya DRC, Thomas Emmanuel Ulimwengu
kabla ya mapumziko.
Ngorongoro Heroesinatarajiwa kurejea nchini
Jumapili (leo) majira ya Saa 3 asubuhi.
Mshindi kati ya Ngorongoro na Nigeria
atamenyana na mshindi kati ya Afrika Kusini na Kongo Brazzaville, mechi ya
kwanza ikichezwa kati ya Septemba 21 na 23 mwaka huu ugenini na marudiano Oktoba
6.
0 comments:
Post a Comment