• HABARI MPYA

    Sunday, May 06, 2012

    MAN UNITED YAICHAPA SWANSEA 2-0


     6 Mei, 2012 - Saa 17:16 GMT
    Alex
    Meneja wa United, Alex Ferguson. Wanahitaji miujiza kutetea unigwa wao
    Manchester United wameendelea kuweka ndoto zao za kutetea ubingwa wao kwa kuichapa Swansea kwa mabao 2-0.
    United walijitahidi kutaka kufunga mabao mengi ili kupunguza tofauti iliyopo kati yao na Manchester City, lakini walipoteza nafasi nyingi za kufanikisha hilo.
    Paul Scholes ndio aliandika bao la kwanza la United huku la pili likifungwa na Ashley Young.
    Manchester City wanaendelea kuongoza ligi wakiwa pointi sawa na United, lakini wana magoli 8 zaidi.
    Manchester City watatangazwa kuwa mabingwa wiki ijayo iwapo wataichapa QPR, hata kama Manchester United watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Sunderland.
    Iwapo United watataka kuchukua ubingwa, watalazimika kupata ushindi wa magoli zaidi ya manane huku wakizingatia matokeo yatakayopatikana kati ya City na QPR.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA SWANSEA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top