![]() |
Thadeo |
MKURUGENZI wa Michezo wa Wizara ya Habari
Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo amesema kwamba wachezaji wa Tanzania
wanacheza tu soka bila ya kuwa ndoto, jambo ambalo limewafanya wasifike mbali.
Akizungumza katika hafla maalum ya
kuwapongeza wachezaji wa Azam FC kwa kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, Thadeo ambaye ni beki wa zamani wa Yanga, amesema kwamba
kutokuwa na ndoto kwa wachezaji wa Tanzania ni tatizo kubwa.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa
na Azam FC kwenye hoteli ya JB Belmonte katikati ya Jiji la Dar es Salaam,
Thadeo aliwataka viongozi kuchangia ndoto zao za kuwa timu tishio Tanzania na
wachezaji wao.
Alisema iwapo Azam itakuwa na ndoto ya
kufika mbali bila ya wachezaji wao na ndoto hiyo itakuwa ni sawa na kuchukua
sukari na kumwaga baharini.
“Lazima wachezaji wa Azam wawe na ndoto ya
kufika mbali, ndipo ndoto za Azam FC zitatimia kwa urahisi,”alisema Thadeo.
Aidha, Thadeo aliwataka Azam wasiogope
mkwara wa Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage ambaye mapema akizungumza
kwenye hafla hiyo, alisema Azam wacheze ligi wakigombea nafasi ya pili tu,
wakithubutu kuchukua ubingwa timu yao itakufa.
“Katika historia, timu zote zilizochukua
ubingwa msimu uliofuata zilishuka na kufa kabisa kasoro Mtibwa Sugar tu, hivyo
nawaomba Azam wacheze ligi wakigombea nafasi ya pili tu kila mwaka,”alisema
Rage.
![]() |
Basi la Azam |
Akimjibu Rage, Thadeo alisema; “Madai kwamba
mkichukua ubingwa timu yenu itakufa, ilikuwa wakati huo, siyo sasa, hizo timu
zilizokufa zilikuwa hazina misingi bora, hazikuwa na academy, hawakuwekeza, ila
Azam iko imara. Nawapongeza sana na nawaomba endeleeni na juhudi zenu hivyo
hivyo.
Pamoja na madai ya Rage, timu zikichukua
ubingwa zinakufa, lakini msimu huu mbali na Mtibwa Sugar, mabingwa mara mbili
mfululizo 1999 na 2000, msimu huu wa ligi ukiacha Simba na Yanga, ulishirikisha
bingwa mwingine wa zamani wa ligi hiyo, Coastal Union ya Tanga waliochukua taji
hilo mwaka 1988.
Timu zilizowahi kuchukua ubingwa na sasa hazipo
kwenye ramani ya soka ni Mseto mwaka 1975 na Tukuyu Stars mwaka 1986, Pan African
imeshuka tu daraja na inapigania kurejea Ligi Kuu, ingawa haina makali ya awali
na hiyo ni kama alivyoseam Thadeo hawajawekeza.
Naye Mwenyekiti wa Azam FC, Abubakar Bakhresa
alilaani hila na njama ilizokuwa ikifanyiwa timu yake masimu huu ili
kuwadhoofisha, ikiwemo kuwapiga marefa wa mechi zao.
Abubakar alisema kwamba pamoja na hila hizo
hawakukata tamaa, walipigana hadi dakika ya mwisho na kufanikiwa kupata nafasi
ya pili kwenye ligi, ambayo itawawezesha kushiriki Kombe la Shirikisho la Soka Afrika
mwakani.
“Soka Tanzania sasa inainuka na imekuwa
ajira nzuri na wachezaji wengi sasa wanavutiwa kucheza Tanzania. Mchezaji anaona
bora kuja kucheza Azam, kuliko kwenda kuhangaika sehemu nyingine.
Wachezaji wa Azam wanalipwa vizuri,
wanaishi vizuri na wanafurahia maisha na ajira yao nzuri,”alisema.
Alisema wakati wanashiriki Ligi Kuu msimu
wa kwanza, ndoto zao zilikuwa kucheza ili kubaki kwenye ligi, lakini msimu wao
wa nne, wanashika nafasi ya pili na hayo wanayachukulia kama mafanikio makubwa.
Alisema mafanikio haya ni mwendelezo wa
mafanikio yaliyoanzia kwenye kutwaa Kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu
visiwani Zanzibar mbele ya vigogo wa soka Tanzania, Simba na Yanga.
Abubakar alisema dhamira ya Azam msimu ujao
ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho.
![]() |
Uwanja wa Azam |
Akimalizia hotuba yake, Abubakar aliwataka
wachezaji wa Azam kutumia vizuri kipindi chao cha likizo kwa kujitunza, ili warejee
msimu ujao wakiwa vizuri. Akaagana kabisa na wachezaji ambao hawatasajiliwa
tena timu hiyo, akisema anawatakia maisha mema popote waendako.
WASHINDI WA TUZO ZA AZAM:
1) OUTSTANDING PLAYER OF THE YEAR
Sr Team- ABUBAKAR SALUM (SUREBOY)
Jr Team – KELVIN FRIDAY
2) BEST ATTITUDE IN TRAINING
Sr.Team – LUCKSON KAKOLAKI
Jr.Team – ISMAIL ADAM GAMBO
3) BEST DISCIPLINED PLAYER ON /OFF THE
FIELD
Sr.Team- VAZIRI OMARI
Jr.Team – ASSAD MUSA
4) MOST PROMISING PLAYER
Sr.Team – HAMIS MCHHA (Vialli)
Jr.Team – ALLY KAIJAGE
5) MOST INSPIRATIONAL PLAYER
Sr.Team – AGREY MORRIS
Jr.Team – ABDUL MGAYA
6) MOTIVATIONAL PLAYER OF THE CLUB
Sr.Team -IBRAHIM S CHIMWANGA(Shikanda)
Jr.Team – REYNA ELLY & MUDHATIR YAHAYA
7) FUNNIEST CHARACTER IN TRAINING
Sr.Team – ERASTO NYONI
Jr.Team –HAMADI JUMA
8) FITTEST CHARACTER IN TRAINING
Sr.Team – SAID MORADI
Jr.Team –MOHAMMAD HUSEIN
9) PLAYER OF THE YEAR
Sr.Team – JOHN BOCCO
Jr Team – JOSEPH KIMWAGA
0 comments:
Post a Comment