• HABARI MPYA

    Saturday, May 05, 2012

    MAYWEATHER ANANUKA FEDHA, AKISHINDA NI BALAA


    Floyd Mayweather ameahidiwa dola za Kimarekani Milioni 32.
    LAS VEGAS -- UNAWEZA kununua nini ukipata dola za Kimarekani Milioni 32? Safi, usiku mkubwa wa leo, baada ya pambano lake na Miguel Cotto kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden, Floyd Mayweather Jr. atajua.
    Kwa mujibu wa Kamisheni ya Michezo ya Nevada, Mayweather amehakikishiwa dola Milioni 32 katika pambano la leo la ubingwa wa Chama cha Ngumi Duniani uzito wa Super Welter, kiwango kikubwa zaidi kihistoria kwa bondia kuahidiwa.
    Pamoja na hayo hiyo ni ahadi tu. Mayweather pya ataondoka nyumbani na kitita kitamu zaidi cha faida. Hakuna anayesema, lakini Mayweather alisema katika mahojiano Jumanne atafikisha kiwango cha dola Milioni 100.
    Hakuna shaka, vyovyote atalipwa fedha nyingi kwa kuiweka rehani rekodi yake ya kutopigwa ndani ya mapambano 42 dhidi ya nyota huyo wa Puerto Rico.
    Ahadi hiyo inavunja rekodi ya ahadi ya dola Milioni 30 za Mike Tyson kwa pambano lake la mwaka 1997 na Evander Holyfield. Cotto ameahidiwa dola Milioni 8, hivyo jumla ya mapato yao dola Milioni 40 ni chini ya kiwango cha dola Milioni 41 walizopewa mabondia Tyson na Holyfield. Holyfield alipata dola Milioni 11 kwa pambano hilo.
    Leonard Ellerbe, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mayweather Promotions, hakusema ni kiasi gani zaidi Mayweather atatengeneza, zaidi ya kusema ni kikubwa.
    Hii ni ahadi kubwa zaidi kwa Nevada katika mapambano makubwa yaliyowahi kufanyika Nevada.
    Kwa thamani ya dola, Mayweather ameweka rekodi, lakini kulinganisha na thamani ya dola kwa sasa, Tyson ndiye ameweka rekodi. 
    Kwa mujibu wa site ya viwango, dola Milioni 30 zilizolipwa mwaka 1997 sasa zinaweza kuwa sawa na dola Milioni 42.9 mwaka 2012.
    Wanaume hao wawili wote walipopimwa uzito walikutwa na kiwango sahihi cha uzito wao, Cotto akipata 154 na Mayweather 151.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAYWEATHER ANANUKA FEDHA, AKISHINDA NI BALAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top