BEKI wa kulia wa Arsenal, Mfaransa Bacary Sagna atakosa fainali za Euro 2012 baada ya kuumia mguu katika mechi dhidi ya Norwich City leo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alitolewa uwanjani baada ya kuanguka uwanjani dakika ya 33 katika mechi ya sare ya 3-3 Uwanja wa Emirates.
Hii ni mara ya pili msimu huu Sagna anaumia mguu huo.
Alikwenda kufanyiwa upasuaji Oktoba baada ya kuumia katika mechi waliyoshinda mechi 2-1 dhidi ya Tottenham .
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alithibitisha kuumia kwa mchezaji huyo katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi.