KAMATI ya Mashindano ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) inatarajiwa kukutana leo (Mei 8 mwaka huu) ambapo pamoja na
mambo mengine itapanga vituo vya Ligi ya Taifa na tarehe ya kuanza ligi hiyo.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba, mikoa
nane imeomba kuwa wenyeji wa ligi hiyo itakayochezwa katika vituo vitatu. Mikoa
hiyo kupitia kwenye vyama vyao vya mpira wa miguu ni
Ameitaja mikoa iliyoomba vituo ni Dar es
Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Mara, Mbeya, Shinyanga na Singida.
Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni mabingwa wa
mikoa. Timu hizo ni Ashanti United ya Ilala (Dar es Salaam), Aston Villa
(Singida), Bandari FC (Kagera), CDA (Dodoma), Flamingo SC (Arusha), Forest FC
ya Siha (Kilimanjaro), JKT Kanembwa (Kigoma), Korogwe United ya Korogwe
(Tanga), Kurugenzi ya Mafinga (Iringa), Lindi SC (Lindi) na Majimaji (Tabora).
Mighty Elephant (Ruvuma), Mkamba Rangers ya
Kilombero (Morogoro), Mpanda Stars ya Mpanda (Rukwa), Mwadui FC (Shinyanga),
Nangwa VTC (Manyara), Ndanda FC (Mtwara), Pamba SC (Mwanza), Polisi Mara
(Mara), Red Coast ya Kinondoni (Dar es Salaam), Super Star ya Bagamoyo (Pwani),
Tenende SC (Mbeya) na Tessema FC ya Temeke (Dar es Salaam).
0 comments:
Post a Comment