SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)
linaitakia kila la kheri timu ya Simba kwenye mechi yake ya marudiano ya Kombe
la Shirikisho Afrika, dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Jumapili
(Mei 13 mwaka huu).
Mechi hiyo itachezwa katika mji wa Shandy
kuanzia saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Simba inaondoka kesho
kwenda huko kwa ndege ya Kenya Airways.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba msafara wa timu hiyo utaongozwa na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TFF, Hussein Mwamba, na unatarajia kurejea nyumbani Mei
15 mwaka huu.
Pia TFF inaipongeza Simba kwa kufanikiwa
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo Mei 6 mwaka huu ilifunga
msimu wa 2011/2012.
0 comments:
Post a Comment