RAiS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou ameelezea mshituko wake
kufuatia kifo cha gwiji wa soka Senegal, Jules Francois Bocande (pichani kushoto).
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba wa Teranga,
amefariki dunia jana (Mei 7) mjini Metz, Ufaransa akiwa na umri wa miaka 53, baada
ya kufanyiwa upasuaji.
Hayatou amekizungumzia kifo hicho kama pigo
linguine kwa soka ya Afrika, kufuatia kifo cha mshambuliaji wa zamani wa
Nigeria, Rashidi Yekini mwishoni mwa wiki.
Hakuna shaka Bocande, alikuwa miongoni mwa
vipaji vya hali ya soka vilivyowahi kutokea Magharibi mwa Afrika na kifo chake
kimekuja saa 72 baada ya kufariki kwa Rashidi
Yekini.
Mshambujliaji huyo alijitengenezea jina
nchini Ufaransa ambako alicheza soka kati ya mwaka 1985 hadi 1986 akifunga
mabao 23 katika klabu ya Metz. Pia alichezea Paris Saint-Germain, OGC Nice na
RC Lens.
Baada ya kustaafu soka, alikuwa kocha wa
muda wa Simba wa Teranga kati ya mwaka 1994 na 195, sambamba na kuwa Mswaidizi
wa Mfaransa, Bruno Metsu katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002 ambako
Senegal ilitinga Robo Fainali.
Mwaka 2009, alitajwa kwenye orodha ya CAF ya
magwiji wa soka Afrika, sambamba na Stephen Keshin wa Nigeria na Osvaldo
Saturnino de Oliviera “Jesus” wa Angola katilka tuzo za Gala zilizofanyika Accra,
Ghana
0 comments:
Post a Comment