Jose Mourinho - Real Madrid
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema kwamba timu yake imezifunga moja ya timu nzuri kihistoria ili kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Hispania, ingawa bado hakubaliani na madai ya timu nyingi kwamba soka ya Barcelona ndio nzuri zaidi.
Ushindi wa Los Blancos 3-0 ugenini dhidi ya Athletic Bilbao Jumatano ulitosha kuwahakikishia ubingwa wa La Liga, wakiizidi Barca pointi saba japo bado mechi mbili ligi kufikia tamati.
Huo ukiwa ubingwa wa kwanza timu hiyo tangu 2008 na wa kwanza kwa Mourinho tangu ajiunge na klabu hiyo 2010, kocha huyo Mreno alijivunia kuzungumzia mafanikio ya timu hiyo.
"Tumefunga moja ya timu nzuri kihistoria, lakini waelewa wanasema cheza soka ambayo tu inaleta mafanikio," alisema.
"Kuna watu wanaoujua mpira kupitia kwenye Google, ambao wanatafuta vitu kwenye kompyuta na kupata uelewa wa soka, lakini soka ni zaidi ya hivyo. Tumecheza soka kubwa, tumefunga mabao mengi na kushinda mechi nyingi."
Taji hilo la La Liga linamaanisha, kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 ameshinda mataji ya ligi katika nchi nne tofauti; mengine Italia alipokuwa na Inter Milan,England na Chelsea na Ureno akiwa na Porto FC.
"Ni mipango niliyokuwa nayo na sasa nimefanikiwa. sasa nimeshinda ligi nilizotaka; ambazo ni wa nchi yangu mwenyewe na wa nchi tatu mujhimu zaidi Ulaya. Sikuwa na malengo ya kushinda ubingwa tofauti. Hakuna ligi nyingine inayonivutia mimi.
"Sijachoka bado. Nahitaji mengi hadi nichoke, hivyo nitaendelea kujaribu kutwaa taji langu la nane la ligi na kuendelea kuogelea kwenye wimbi la furaha."
Madrid inarejea kwenye La Liga Jumamosi itakapocheza ugenini na Granada

.png)
0 comments:
Post a Comment