SOKA | LIGI KUU ENGLAND...
BAO la tik tak la Wayne Rooney aliloifungia Manchester United dhidi ya Manchester City, Februari msimu uliopita limepigiwa kura na mashabiki kama bao bora kwa miaka 20 ya Ligi Kuu ya England, imetangazwa leo.
Bao hilo la Rooney lililoipa United ushindi wa 2-1 nyumbani na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, lilikuwa bao pekee lililopigiwa kra katika mabao yote ya miaka 10 yaliyopendekezwa.
Bao la Dennis Bergkamp akiichezea Arsenal dhidi ya Newcastle United mwaka 2002 na mchezaji mwenzake Thierry Henry alilofunga dhidi ya Manchester United mwaka 2000 yalishika nafasi ya pili na ya tatu.
Ligi Kuu imesema katika taarifa yake mamia kati ya malefu waliopiga kura mabao hayo matatu yalipata zaikdi ya nusu ya kura, huku Rooney akipata asilimia 26, Bergkamp 19 na Henry 15.
"Nimekua naangalia Ligi Kuu, hivyo kuchaguliwa kwa bao langu kuwa la kihistoria katika Ligi Kuu ni hisia kubwa," alisema Rooney.
"Ningependa kuwashukuru mashabiki wote walionipigia kura."
Mchezaji wa zamani wa United, David Beckham alishinda tuzo ya miaka 10, mwaka 2002 kwa bao lake kutoka katikati ya Uwanja dhidi ya Wimbledon mwaka 1996.
Tuzo hizo zinahusisha pia mechi bora, kuokoa na mshangiliaji bora wa bao na kura hupigwa kwa njia ya mtandao.
Rooney alishindwa kurudia cheche hizo Jumatatu wakati City ilipoifunga United 1-0 na kufufua matumani ya ubingwa.


.png)
0 comments:
Post a Comment