Mwenge wa Olimpiki
Mwenge wa Olimpiki
MOTO wa mwenge utakaotumiwa kuasha mwenge
wa mashindano ya Olimpiki mjini London uliashwa mahali yalipozaliwa mashindano
ya kale ya Olimpiki siku ya Alhamisi.
Muigizaji mwanamke, aliyevalia kama mtawa
mwanamke wa enzi za miungu wa Kigiriki alitumia kiyoo kupokea mwanga wa jua na
kuasha mwenye.
Kukiwa na jua la kutosha angani, hapakua na
sababu ya kutegemea moto kutoka kwingine wakati wa kufanya majaribio ya mwisho
kuasha mwenge wa Olimpiki siku moja kabla.
Baada ya sherehe za kufana, mtawa huyo
atakabidhi mwenge kwa mtu wa kwanza kutembeza mwenge huo, mwanariadha
muogeleaji kutoka Ugiriki aliyeshinda medali ya fedha kwenye mashindano yya
Olimpiki Spyros Gianniotis.
Gianniotis ni mmoja wa watu 490
watakaotembeza mwenge huo mwendo wenye umbali wa kilomita 2,900 kupitia Ugiriki
kabla haujakabidhiwa kwa watayarishaji wa mashindano ya London tareh 17 Mayyy.
Tafauti na tabia ya mashindano ya awali,
ambapo mwenge huu unazungushwa dunia nzima, safari hii utavuka nje ya visiwa
vya Uingereza mara moja u, kupitia Dublin mnamo tareh 6 Juni.
Mashindano ya Olimpiki yataanza tareh 27
Julai hadi tareh 12 Agosti 2012.


.png)
0 comments:
Post a Comment