WAKATI kukiwemo na taarifa za baadhi ya
wachezaji nyota wa klabu ya Yanga kutemwa, mshambuliaji wa timu hiyo Jerry
Tegete anadaiwa kusaini mkataba wa kuichezea Simba katika msimu ujao wa ligi na
michuano ya kimataifa. Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam, zinaeleza
kuwa Tegete ambaye ni mmoja ya wachezaji waliopigiwa mstari katika klabu ya
Yanga amefikia uamuzi baada ya mkataba wake kumalizika huku kukiwa na uwezekano
mdogo wa kuongezewa mkataba. Hivi karibuni hali ndani ya klabu hiyo yenye
maskani yake mitaa ya Janwani na Twiga imeonekana kubwa tete baada ya timu hiyo
kupoteza mwelekeo na hatimaye kuutema ubingwa wake uliokwenda kwa mahasimu wao
wa jadi nchini Simba. Kama hiyoi haitoshi mambo yalizidi kuwa mabaya baada ya
Yanga kuchapwa mabao 5-0 na Simba katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu soka
Tanzania Bara ambapo Yanga ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 42,
nyuma ya Azam iliyomaliza ikiwa na pointi 56 na Simba iliyomaliza ikiwa na
pointi 62. Kwa mantiki hiyo, uongozi umepanga kukisafisha kikosi chake hivyo
baadhi ya wachezaji kuwa hatarini kutemwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
kushuka kiwango, nidhamu mbovu wakiwemo Tegete, Shamte Ally, Chacha Marwa,
Mohamed Mbegu, Abuu Ubwa, Zuberi Ubwa, Kigi Makasi, Shadrack Nsajigwa na Athuman
Idd 'Chuji'. Tegete anahusishwa kwenda Simba, wakati Nsajigwa anatuhumiwa
kucheza chini ya kiwango katika mechi yao dhidi ya Simba, ambapo alisababisha
penalti mbili kati ya tatu na kuwapa mahasimu wao ushindi wa mabao 5-0,
wachezaji wengine wakiwa wamemaliza mikataba yao, ingawa ndani yake Chuji
huenda akaongezwa mkataba. Hata hivyo wachezaji kama Nurdin Bakari, Hamis
Kiiza, Kenneth Asamoah bado wana mkataba wa mwaka mmoja, wakati Yaw Berko na
Davis Mwape mikataba yao itamalizika Novemba mwaka huu na uongozi umeshaanza
kuzungumza na kuzungumza na Berko kuangalia uwezekano wa kuongeza mkataba wake,
lakini Mwape hatacheza Yanga msimu ujao mara baada ya mkataba wake kumalizika.
SOURCE: DINA ISMAIL
(mamapipiro.blogspot.com)



.png)
0 comments:
Post a Comment