Na Lucy Mgina
MWENYEKITI wa Yanga, Lloyd Nchunga, amewataka wazee wa klabu hiyo watulie na kuwataka wakaangalie wanavyommaliza Mnyama keshokutwa Jumapili katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Nchunga ameliambia Championi Ijumaa kuwa wazee wa klabu hiyo hawapaswi kulalamika katika kipindi hiki wanachoelekea katika mechi dhidi ya Simba, isipokuwa watulie na wawaunge mkono.
“Unajua wao wanalalamika eti nimeuza mechi dhidi ya Simba, sasa nawaambia hicho kitu hakuna, kwani hao walipokuwa viongozi walikuwa wakifanya mchezo huo wa kuuza mechi? Ni jambo ambalo haliwezekani.
“Nina matarajio makubwa ya kufanya vizuri katika mechi hiyo kwa kuwa tuna kikosi imara na mpaka sasa timu ipo kambini, ” alisema Nchunga.
Hivi karibuni, baadhi ya wazee wa Yanga walitaka kuchukua majukumu ya kuiongoza timu hiyo kutoka kwa Nchunga kwa kile kilichoonekana alishindwa kuiendesha, lakini mwenyekiti huyo alitupilia mbali maneno hayo na kusema klabu bado ipo chini ya uongozi wake.

GAZETI LA CHAMPIONI

.png)
0 comments:
Post a Comment