8 Mei, 2012 - Saa 13:45 GMT
| Chisora kushoto na Haye kulia. |
MABONDIA David Haye na Dereck Chisora
wanatazamiwa kupanda ulingoni na kupambana Julai 14, mwaka huu katika pambano
lililoidhinishwa na Shirikisho la ngumi la Luxemboug.
Meneja wa Chisora, Frank Warren, amesema
pambano hilo litafanyika katika mtaa wa Upton Park, Uingereza.
Mabondia hao wawili wa uzani wa heavy
waligombana na kuanza kumenyana katika mkutano wa waandishi wa habari, mara tu
baada ya Chisora kutandikwa mjini Munich na bondia Vitali Klitschko mwezi
Februari.
Bodi ya mchezo wa ngumi nchini Uingereza
ilikataa kuidhinisha pambano hilo, kwani mabondia wote wawili hawana leseni ya
Uingereza inayowaruhusu kupambana.
Uamuzi kufuatia rufaa ya Dereck Chisora
kutetea uamuzi wa kumpokonya leseni umecheleweshwa, na Frank Warren
amekasirishwa sana na namna bodi ya Uingereza ya ngumi ilivyoshughulikia suala
hilo.
“Kwa wengi ni vigumu kuvumilia kuwaona
Chisora na David Haye hatimaye wakinufaika kutokana na tukio la fedheha mjini
Munich, lakini katika ngumi, tukio kama hilo ni chanzo cha pambano la kusisimua
zaidi litakaloweza kufanyika katika nchi hii”.
Chisora alipokonywa leseni kufuatia matukio
kadha kabla na baada ya pambano lake dhidi ya Klitschko.
Kati ya matukio hayo, Chisora, mwenye umri
wa miaka 28, alimpiga kofi Klitschko kutoka Ukraine, wakati mabondia hao wawili
walipokuwa wakipimwa uzani, na kisha kumtemea maji ndugu yake, Wladimir, kabla
ya pambano hilo.
Kwa upande wake, Haye aliisalimisha leseni
yake mwezi Oktoba mwaka jana, miezi mitatu baada ya kushindwa na Wladimir mjini
Hamburg, Ujerumani, katika pambano la kuwania mkanda wa WBA.
Awali Warren alikuwa amesema hana nia ya
kusimamia pambano kati ya Chisora na Haye.
Lakini amesema amebadilisha nia, kwa kuona
rufaa ya Chisora kutaka leseni sasa imesukumwa hadi mwezi Julai.
Warren anakiri kwamba alilofanya Chisora ni
jambo la kipumbavu, na anastahili adhabu.
Lakini anasema bondia huyo atakuwa nje ya
ulingo miezi sita, na ana haki ya kujipatia pesa na riziki yake maishani


.png)
0 comments:
Post a Comment