Pichani ni washiriki 40 wa kozi iliyokamilika Zanzibar Mei 7, mwaka huu. |
SHIRIKISHO la mpira wa Wavu la Taifa (TAVA)
linaendesha mpango wa maendeleo wa mpira wa wavu nchini kwa kuendesha mafunzo
ya ndani ya mchezo huo kwa makocha ambao ni waalimu wa michezo wa shule za
msingi na sekodari nchini. Alfred Selengia.
Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo mpira wa
wavu TAVA, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mpango huo wenye jina la mradi hapo
juu umefadhiliwa na shirikisho la dunia la mpira wa wavu FIVB katika mfuko wake
wa maendeleo. (FIVB DEVELOPMENT FUND).
TAVA imefadhiliwa na mfuko huo, vifaa
vyenye jumla ya thamani zaidi ya sh.Milioni 140 vikiwemo mipira na net za
kuchezea.
Kupitia mradi huo uliobuniwa na TAVA, TAVA
itaendesha mafunzo hayo karibu katika mikoa yote ya Tanzania kwa kuanzia na
mikoa kumi ya awali ambayo ni Dar, Tanga,Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza,
Morogoro, Dodoma, Kagera na Zanzibar. Mafunzo hayo tayari yameshafanyika
Zanzibar na sasa yanaendelea Tanga na Manyara. Lengo nikufikia zaidi ya waalimu
600 ambao kila mwalimu akifundisha vijana 20 basi zaidi ya vijana 10,000
watakuwa wamenufaika na Mradi huu.
Lengo hasa la TAVA ni kuwa na msingi mzuri
wa wachezaji wa baadae hapa nchini. Ni ukweli usiofichika kuwa ni kupitia shule
za msingi na sekondari ndipo vipaji vya mchezo wetu uvumbuliwa. Hivyo kwa
kuzingatia hilo ni matarajio yetu makubwa kuwa miaka ya mbeleni tutakuwa na
wachezaji wengi wazuri waliotoka katika mikono ya waalimu waliopitia mafunzo
yetu.
Lengo lingine la TAVA ni kuanzisha na
kuimarisha vyama vya mikoa kwa kuwasaidia vifaa vyama vyote vilivyo hai kwa
ajili ya kuendesha na kukuza mchezo wetu katiaka mikoa yao.
TAVA inatoa rai kwa waalimu wote watakao
nufaika na mradi huu, kuwa chachu ya maendeleo ya mchezo weto kwa kufanyia kazi
kwa moyo, upendo na kwa kujitolea kuwafunza vijana wao mashuleni ili lengo letu
lifikiwe. Vile vile kuwaomba wakuu wa mashule, Maafisa Elimu wa Mikoa, na wadau
wote wa michezo kutoa ushirikianao wa hali ya juu katika kuwaruhusu na
kuwawezesha waalimu kushiriki mafunzo hayo punde yanapofika katika mikoa yao.
Aidha TAVA inashukuru Baraza la michezo la taifa kwa kuwezesha kupokea vifaa
vyote vilipofika chini na kuvitunza hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment