FRANK SANGA, Mwanaspoti
KOSTA Papic amemchagua mchezaji bora wa
mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga na kumtetea mwamuzi wa mchezo
kuwa aliumudu mchezo.
Katika mahojiano na Mwanaspoti jana
Jumatatu, Papic alisema Emmanuel Okwi ni mchezaji Bora wa mchezo huo.
Mwanaspoti: Kwa ujumla uliuonaje mchezo wa
Simba na Yanga?
Papic: Yanga walicheza vizuri kipindi cha
kwanza, lakini wakashindwa kufunga. Kipindi cha pili walikufa kabisa na Simba
wakatumia mwanya huo.
Nadhani kwa ujumla Simba walicheza vizuri
kuliko Yanga, lakini mabao 5-0 yalikuwa mengi mno.
Mwanaspoti: Uliridhika jinsi kikosi cha
Yanga kilivyopangwa?
Papic: Kocha (Minziro) aliyekuwa na Yanga
kambini anajua vizuri zaidi, amekuwa na wachezaji kwa siku zote kwa hiyo alijua
alichokifanya. Mimi sikuwa na kibali cha kufanya kazi. Hilo nadhani kocha
aliyekuwapo anajua zaidi.
Mwanaspoti: Unadhani nani alikuwa mchezaji
bora wa mechi?
Papic: Hilo halina ubishi Okwi.
Amesababisha mabao yote matano.
Mwanaspoti: Unadhani anaweza kucheza Afrika
Kusini au Ulaya?
Papic: Aende Ulaya, soka lake ni kubwa,
tatizo jingine ni kuwa akienda Afrika Kusini ni ngumu kwenda Ulaya, ila akienda
Ulaya anaweza kuanza na timu ndogo baadaye akapata timu kubwa.
Mwanaspoti: Vipi mwamuzi wa mchezo?
Papic: Alichezesha vizuri sana. Yanga imefungwa
mabao matano, lakini hakuna sehemu unaweza kumlaumu mwamuzi. Alifanya kazi
nzuri.
Mwanaspoti: Ungekuwa benchi la Yanga
ungeweza kubadilisha matokeo?
Papic: Swali zuri, lakini siwezi kukujibu.
Mkataba wangu umekwisha na Yanga. Ila kila kitu kingekuwa kizuri kama wachezaji
wangekuwa wanalipwa mishahara yao na kocha angekuwa analipwa na kutafutiwa
kibali cha kazi.
Mwanaspoti: Unashauri Yanga wafanye usajili
wa nafasi zipi?
Papic: Siwezi kutoa ushauri, sasa nafikiria
kujiunga na timu nyingine. Lakini Yanga ina matatizo mengi.
Mwanaspoti: Unajiunga na timu gani?
Papic: Siwezi kusema hapa, pengine unajua
0 comments:
Post a Comment