Na Khatimu Naheka
ZIKIWA zimesalia saa takribani 48 kabla ya kufikia tamati ya Ligi Kuu Bara 2011/12, kipa wa Simba, Juma Kaseja, ndiye shujaa baada ya kucheza michezo yote 25 iliyopita akiwa na klabu yake kwa muda wa dakika 90 kwa kila mechi.
Kaseja, nahodha wa kikosi hicho, amecheza muda wote huo ambao ni sawa na dakika 2,250 kwa mechi 25, akiwa amefungwa mabao 12 na kuiwezesha timu yake kufikisha pointi 59 kileleni.
Hayo ni mafanikio mengine kwa kipa huyo wa zamani wa Moro United ambaye amekuwa kwenye kikosi cha kwanza klabuni hapo kwa kipindi cha miaka tisa mfululizo, japo kuna msimu mmoja ambao alihamia Yanga kisha akarejea Simba.
Wakati hali ikiwa hivyo, beki wa Simba, Derrick Walulya, raia wa Uganda, alicheza mechi mbili, ambapo moja alimaliza dakika 90 huku nyingine akitumia dakika 75, hivyo kuwa amecheza dakika 165 mpaka sasa.
Beki wa Azam, Aggrey Morris, amecheza mechi 24 na ametumia jumla ya dakika 2,160 kuwa uwanjani.

.png)
0 comments:
Post a Comment