Sinkala |
TOUT Puissant Mazembe imefuzu kuingia Nane
Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa mara ya sita mfululizo baada ya kutoa sare
ya 1-1 na wenyeji El Merreikh kwenye Uwanja wa Omdurman, Khartoum jana, Mazembe,
yenye mshambuliaji mwingine Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu, lakini ‘anasugua
mwanzo mwsiho’, ilitangulia kupata bao kupitia kwa Nathan Sinkala.
Mazembe imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-1,
baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani, Mbwana Ally Samatta wa Tanzania akifunga
bao moja.
Merreikh ilisawazisha kupitia kwa mchezaji
wake Mganda, Mike MUTYABA dakika ya 61.
Kama kawaida, mshambuliajio chipukizi wa
Tanzania, Mbwana Ally samatta alikuwa mwiba mchungu kwenye safu ya ulinzi ya
Merreikh na hata bao la jana lina mchango wake.
Sasa ni wakati wa Samatta kujiuza zaidi kupitia mechi sita atakazocheza kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa- na kutokana na ndoto za Mazembe kuchukua ubingwa, kuna uwezekano kinda huyo wa Tanzania mwishoni mwa mwaka akaweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
0 comments:
Post a Comment