• HABARI MPYA

    Sunday, May 13, 2012

    UNAYOPASWA KUJUA KABLA YA MAN CITY V QPR LEO

    Aguero


    VIKOSI VYA LEO:


    MANCHESTER CITY


    Hart
    Zabaleta, Kompany, Lescott, Clichy Yaya Toure, Barry
    Nasri, Silva
    Aguero, Tevez
    QPR

    KennyOnuoha, Ferdinand, Hill, Taiwo
    Mackie, Barton, Derry, Taarabt
    Zamora, Cisse


    IKIWA haina mchezaji majeruhi au anayetumikia adhabu, kocha Roberto Mancini hana cha kuhofia akiwa kikosi kamili katika mechi ya mwisho ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England, dhidi ya QPR Uwanja wa Ethiad leo.
    Kwa sababu hiyo, hatutarajii mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester City ikitarajiwa kushusha kikosi kile kile kilichozifunga Manchester United na Newcastle katika mechi mbili zilizopita.
    Kwa QPR, wote Shaun Derry anayesumbuliwa na maumivu ya mguu na Akos Buzsaky nyama za paja, wako shakani kucheza, ingawa kocha though Mark Hughes anaweza 'kuwatoa muhanga' ili kuimarisha safu yake ya kiungo katika mchezo wa leo mgumu wanaotakiwa kushinda wabaki Ligi Kuu.
    Samba Diakite anayesumbuliwa na virusi, dhahiri ataukosa mchezo huo, wakati Alejandro Faurlin ataendelea kuwamo kikosini licha ya maumivu ya mguu yanayomkabili. Djibril Cisse, aliyefunga bao muhimu pekee la ushindi dakika za mwishoni dhidi ya Stoke City katika mchezo uliopita ugenini, anaweza kuwamo kwenye kikosi cha kwanza.


    JE, WAJUA?

    • 1.      Manchester City wana nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa, kwani hata Manchester United wakiifunga Sunderland, wao wakawafunga QPR kipigo kiduchu, wanajivunia wastani wa mabao tisa zaidi walioyonayo hadi sasa dhidi ya wapinzani wao hao.

      2.    Kikosi cha Roberto Mancini, kimeshinda mechi zao 17 za nyumbani hadi sasa, na matokeo mbaya Etihad hadi sasa ni sare ya 3-3 na Sunderland, Machi 31.

      3.    Mshambuliaji wa City, Sergio Aguero amefunga mabao mengi zaidi Ligi Kuu msimu huu (22) ambayo ni mabao manne zaidi katika idadi ya jumla ya mabao ya QPR waliyofunga msimu huu.

      4.   Wenyeji wameshinda mechi zao zote tano zilizopita, wakitisa nyavu za wapinzani mara 15 ndani ya mechi hizo na zao kutikiswa mara moja tu.

      5.   QPR wamefungwa mechi 10 zilizopita kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Stoke City katika mechi iliyopita.
      6.    Pointi tatu zitaihakikishia QPR. Sare pia itawasaidia kunusurika kwa wastani mzuri wa mabao - lakini kikosi cha Mark Hughes kikifungwa na Bolton ikaifunga Stoke, wageni watarejea Championship.

      7.    Tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Lazio, Januari, Djibril Cisse (pichani juu kulia)  amekuwa akifunga mabao sambamba na kupigwa kadi nyekundu, hadi sasa akiwa amefunga mabao matano na kupewa kadi mbili nyekundu.

      8.    Kocha wa QPR, Hughes aliiongoza City kwa miezi 18 kati ya mwaka 2008 na 2009 kabla ya kupigwa chini na nafasi yake kupewa Mancini.

      9.    Man City wana kawaida ya kuuanza mchezo mtaratibu, huku asilimia nane tu ya mabao yao ndiyo yamepatikana katika dakika 20 za mwanzo kwenye Ligi Kuu, wakati QPR asilimia 25 ya mabao yao ni ya mapema..

      10.                       Yaya Toure alifunga bao la ushindi katika ushindi wa 3-2 wa City mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Loftus Road,Novemba 5, mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UNAYOPASWA KUJUA KABLA YA MAN CITY V QPR LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top