KIPA wa Mtibwa Sugar, Deo Munishi ‘Dida’ aliyewahi kuchezea Simba SC, amesajiliwa Azam FC akiwa miongoni mwa wachezaji wawili wapya pamoja na kiungo
Mkenya George Odhiambo ‘Blackberry’.
Azam imesajili wachezaji 27- huku wanne kati
yao wakiwa katika hesabu za kutolewa kwa mkopo akiwemo kiungo Zahoro Pazi
anayepelekwa Coastal Union ya Tanga- maana yake itabaki na wachezaji 23.
Jumla, Azam imesajili wachezaji wanne wa
kigeni na kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu wana nafasi moja ya kusajili
mchezaji wa kigeni na tayari rada za klabu hiyo zimemlenga mshambuliaji wa
Simba SC, Emmanuel Okwi ambaye yuko juu hvi sasa hakuna mfano.
Wachezaji wa kigeni wa Azam ni beki Ibrahim
Shikanda kutoka Kenya, viungo Blackberry kutoka Kenya, Kipre Balou na mshambuliaji
Kipre Tcheche, wote kutoka Ivory Coast.
Aidha, Azam FC imezikata maini Simba na
Yanga zilizokuwa zinamuwania beki wao, Luckson Kakolaki aliyekulia kwenye
viunga vya wana Lamba Lamba, ambaye amesani wiki hii.
Azam FC ambayo itawakilisha nchi kwenye,
ambayo mwakani itacheza Kombe la Shirikisho Afrika, pia imewapandisha chipukizi
wake wane kutoka timu ya vijana (U-20), ambao ni Aishi Salum, Jackson Wandwi,
Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph Kimwaga
Kikosi kamili cha washindi hao wa Medali ya
Fedha Ligi Kuu na mabingwa wa Kombe la Mapinduzi ni; Makipa Mwadini Ally, Deo
Munishi, Aishi Salum na Jackson Wandwi, mabeki Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni,
Waziri Salum, Samih Haji Nuhu, Luckson Kakolaki, Said Moradi, Joseph Owino na
Aggrey Morris na viungo Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum
Abubakar, Abdi Kassim Sadallah, Ramadhani Suleiman Chombo, Abdulghani Ghulam,
Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, Ibrahim Joel Mwaipopo, Kipre Tchetche,
Mrisho Ngassa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha na George Odhiambo, wakati washambuliaji
wa ni Gaudence Mwaikimba na John Raphael Bocco ‘Adebayor’.
0 comments:
Post a Comment