• HABARI MPYA

    Sunday, May 13, 2012

    MUNGU IBARIKI SIMBA SC LEO


    Kikosi cha Simba
    WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC leo wana kazi moja tu ya kumalizia kazi waliyoifanya kwa kiasi kikubwa Dar es Salaam, wiki mbili zilizopita.
    Simba leo itakuwa uwanjani Sudan kumenyana na Al Ahly Shendi ya huko katika mechi ya pili ya raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
    Simba iliondoka jijini Jumanne kuelekea Sudan kwa ajili ya mechi hiyo ambapo hata hivyo hawakupata mapokezi mazuri kutoka kwa wenyeji wao hali ilioufanya uongozi wa klabu
    hiyo kuazimia kupeleka malalamiko (CAF).
    Simba leo inahitaji ushindi au kama kufungwa isiwe zaidi ya mabao 3-0 ili isonge mbele hatua inayofuata ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
    Habari kutoka Sudan zinasema pamoja na vituko walivyofanyiwa na wenyeji, lakini kikosi cha Simba kiko imara kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa katika mji wa Shendi.
    Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga Simba imefanyiwa vitendo ambavyo si vya kiuanamichezo ikiwa ni pamoja na kusafirishwa umbali mrefu, kupewa chakula usiku sana pamoja na kulazwa kwenye hosteli badala ya hoteli nzuri kama walivyofanyiwa wao
    walipofika nchini.
    Kamwaga alisema wachezaji wako kwenye hali nzuri na kocha Milovan Circovick ameahidi kuibuka na ushindi.
    “Kila kitu chetu kwa upande wa benchi la ufundi kiko sawa, pamoja na vurugu zao lakini tunaamini dakika 90 uwanjani ndio zitaongea,” alisema Kamwaga.
    “Wachezaji wako kwenye ari kubwa pamoja na mizengwe ya hapa na pale, kwani hawakukatishwa tamaa badala yake walifanya mazoezi wenyewe pamoja na kocha kuwapa
    mapumziko… wachezaji wanasema lengo lao ni kuvuka raundi inayofuata na watavuka hata wakiwafanyiwa vituko,”alisema Kamwaga.


    VIKOSI VYA LEO:
    SIMBA SC:
    Kikosi cha Simba leo kinatarajiwa kuwa; Juma Kaseja. Shomari Kapombe, Amir Maftah, Victor Costa, Kelvin Yondan, Mwinyi Kazimoto, Uhuru Suleiman, Patrick Mafisango, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Emmanuel Okwi, wakati kwenye benchi watakuwapo Ally Mustafa
    ‘Barthez’, Obadia Mungusa, Juma Jabu, Derrick Walullya na Salum Machaku.

    Al AHYL SHANDY:
    Abdulrahma Ali, Elnour Altigani, Isaac Seun Malik, Saddam Abu Talib, Fareed Mohamed/Orwah Ibrahim dk 83, Zakaria Nasu, Razak Yakubu, Faris Abdallah, Hamopuda Bashir/Mogabid Farouq dk63, Nadir Eltaveb na Bashiro Ubamba.  

    Mungu ibariki Simba. Ibariki Tanzania. Amiiin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUNGU IBARIKI SIMBA SC LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top