Habari zilizopatikana kutoka Nairobi na kukaririwa kwenye mtandao wa, SuperSport.com zimeeleza kuwa mchezaji huyo raia wa Tanzania, amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kuchezea timu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hizo, uamuzi huo wa Kinje kujiunga na Simba una nia ya kumuwezesha kuonesha kiwango chake ili aweze kuchezea timu ya soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', ambayo ndiyo ndoto yake kubwa. Kocha Mkuu wa AFC Leopards inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, Jan Koops amethibitisha kuondoka kwa mshambuliaji huyo ambaye pia humudu nafasi zote za kiungo na kusema kuwa hana muda mrefu watamkosa wakati wa kipindi cha usajili mwezi ujao. Alisema Kinje alimjulisha jana kwamba amepata dau zuri Simba na anaondoka na kwamba amewasisitiza anahitaji kurudi nyumbani kucheza soka. "Amenijulisha amepata ofa nzuri Simba na anaondoka, yeye ni Mtanzania anahitaji kurudi kwao kucheza soka. “Ni mchezaji mzuri, tunapoteza mtu muhimu, alikuwa zaidi ya mchezaji, alikuwa nahodha msaidizi na ndiyo utakapoelewa tumepoteza mchezaji wa aina gani," alisema kocha huyo. Kinje ambaye amepata kuchezea Sofapaka ya Kenya, kuna wakati aliripotiwa kutakiwa kuitwa timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars', wakiamini alikuwa Mkenya, lakini uamuzi huo haukutekelezwa kutokana na yeye kuwa raia wa Tanzania na hakuwa tayari kuupoteza. |
Ekiti PDP: No weak candidate for 2026 guber race
-
From Priscilla Ediare, Ado-Ekiti As the race for the 2026 governorship
election gathers momentum in Ekiti State, the Peoples Democratic Party
(PDP) has s...
51 minutes ago
0 comments:
Post a Comment