Tetesi za J'pili magazeti ya Ulaya


MAN CITY WAJUNJA REKODI YA DUNIA YA USAJILI

KLABU ya Manchester City imeweka rekodi ya dunia kwa kutaka dau la pauni Milioni 80 kutoka kwa Real Madrid, wanaomtaka mchezaji wao, David Silva.
KOCHA anayekuja Tottenham, Andre Villas-Boas yuko tayari kumsajili winga wa Arsenal, Theo Walcott.
KOCHA wa FC Twente, Steve McLaren amesema amekataa ofa ya kumuuza Luuk De Jong, mwenye umri wa miaka 21,  kwenda Newcastle.
KLABU ya LA Galaxy inataka kumsajili kiungo Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 34, na anaweza kuhamia klabu hiyo kwa sababu Muingereza mwenzake, David Beckham yupo huko.
KLABU ya Swansea City inataka kumsajili beki wa kati wa Hispania, mwenye thamani ya pauni Milioni 3, Jose Manuel 'Chico' Flores, mwenye umri wa miaka 25,kutoka Genoa ya Italia.
KOCHA mpya wa Birmingham, Lee Clark ana wachezaji 14 tu wa kikosi cha kwanza na ameelekeza nguvu zake katika kusajili wachezaji wapya.
WACHEZAJI Stephen Carr na Colin Doyle wanajipanga kubaki Birmingham baada ya kupewa mikataba mipya.
KIPA Ben Foster amesema West Brom's "usuhiano wake maalum" na mashabiki ndiyo siri ya kuhamia kwake Hawthorns.
Frank Lampard
Frank Lampard anaweza kumfuata David Beckham LA Galaxy
KLABU ya Arsenal inataka kumsajili kipa wa Palmero, Emiliano Viviano, mwenye umri wa miaka 26.
KOCHA mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers anataka kumsajili kiungo wa Rangers, Steven Davis, mwenye umri wa miaka 27, ambaye yuko huru kwa sasa.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Tottenham na West Ham, Fredi Kanoute, mwenye umri wa miaka 34, amejiunga na Beijing Guoan ya China kwa mkataba wa miaka miwili.
EURO 2012
KOCHA wa Italia, Cesare Prandelli anafurahi kwamba sasa Mario Balotelli hatimaye anasikiliza ushauri kutoka kwa wale ambao wanataka kumsaidia.
Mario Balotelli
Mario Balotelli alijiunga na Man City kwa pauni Milioni 22 kutoka Inter
KIPA wa Hispania, Iker Casillas ametaja Gianluigi Buffon kama shujaa wake.
Bryan Robson ametetea kiwango cha Wayne Rooney katika Euro 2012, akisema vyombo vya habari havimtendei haki kumuandama.
NAHODHA wa England, Steven Gerrard amesema anaamini wote (England) wanatarajia makubwa kuliko uwezo wa mshambuliaji Wayne Rooney.
RAIS wa UEFA, Michel Platini bado anapinga sheria ya teknolojia kutumika kwenye mstari wa lango, licha ya Ukraine kukataliwa bao halali dhidi ya England katika Euro 2012.

WILSHERE BALAA TUPU

KIUNGO wa Arsenal, Jack Wilshere ataukosa mwanzo wa msimu na pia anaweza kukosa mechi ya kwanza ya England kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Italia, Gianfranco Zola anajiandaa kwa mazungumzo ya kuwa kocha wa Watford, baada ya familia ya Pozzo kukamilisha manunuzi ya pauni Milioni 20 ya klabu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza, maarufu kama Championship.