• HABARI MPYA

    Sunday, July 01, 2012

    SIMBA NA EXPRESS LEO TENA


    Simba msimu uliopita

    Na Prince Akbar
    MABINGWA wa soka Tanzania, Simba SC jioni ya leo wanashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na mabingwa wa Uganda, Express ‘Red Eagles’.
    Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ‘Me Liverpool’ ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba maandlizi ya mechi hiyo yamekamilika na amewataka wapenzi wa Simba kumiminika wingi uwanjan kushuhudia nyota wao wapya.
    Kamwaga amesema mshambuliaji wao, ambaye wapo mbioni kumuuza Italia, Mganda Emmanuel Okwi naye atakuwapo joni.
    kamwaga amesema katika mchezo wa leo, Simba itashusha kikosi chake kamili, tofauti na kile kilichotoka sare ya 1-1 katika mchezo wa awali na Tai Mwekundu wa Kampala wiki iliyopita mjini Mwanza. 
    Baada ya mechi hiyo, Simba itavuka maji kwenda kwenye michuano ya Kombe la Ujirani Mwekma inayoandaliwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA EXPRESS LEO TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top