• HABARI MPYA

    Sunday, July 01, 2012

    SERENGETI FIESTA SUPER NYOTA ILIVYOFANA M BEYA


    Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 "Bhaasi" Bwana Sebastian Maganga akiwapongeza washindi wa Serengeti  Fiesta Super Nyota Super J. kulia na Neylee, mara baada ya wasanii hao  kuibuka washindi katika shindano hilo lililofanyika usiku huu kwenye klabu ya Vibes jijini Mbeya, wasanii hawa watauwakilisha mkoa wa Mbeya katika matamasha mbalimbali ya Serengeti Fiesta mikoani
    Mtangazaji wa Clouds Antu Mandoza akizungumza jambo mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao za kreti mbili za bia aina ya Serengeti Lager kutokana na ushindi wao katika shindano hilo lililomalizika usiku hu jijini Mbeya.
    Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Bw. Sebasttian Maganga akitangaza washindi katika shindano la Serengeti Fiesta Super Nyota lililomalizika usiku huu kwenye klabu ya Vibes jijini Mbeya.
    Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kwenye klabu ya Vibes ili kushuhudia shindano hilo wakifuatilia kwa makini wakati wasanii hao walipokuwa wakishindana.
    Msanii Super J. akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki waliojitokeza katika klabu ya Vibes usiku huu.
    Msanii 1 Rich akionyesha uwezo wake jukwaani wakati wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva waliposhindana kuimba katika shindano la Serengeti Fiesta Super Nyota lililomalizika usiku huu kwenye klabu ya Vibes jijini Mbeya
    Mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakiwashangilia wasanii walipokuwa wakishindana katika shindano la Serengeti Fiesta Super Nyota.
    Kutoka kulia wa pili ni Shafii Daudam Sebastian Maganga na Antu Mandoza wakifurahia jambo pamoja na mshabiki wengine waliohudhuria katika shindano hilo.

    Mashabiki wapata burudani ya muziki kabla ya kuanza kwa shindano hilo.

    Saturday, June 30, 2012

    Shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 lafanyika jijini Arusha leo,kundi la Contagious Crew lajinyakulia kitita cha sh. milioni moja


    Mmoja wa majaji wa shindano la  Serengeti Dance la Fiesta 2012 lililofanyika kwenye Club ya Mawingu jioni ya leo,jijini Arusha ,Hamis Mandi a.k.a B Dozen kutoka kipindi cha XXL kinachorushwa na redio ya Clouds FM,akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa kundi shindi la shindano hilo liitwalo Contagious Crew


    Mwendesha shindano hilo pichani kati,Nikson akisoma majina ya makundi mawili yaliyoingia fainali na hatimae kulipata kundi moja mahiri kabisa na kundi la Contigious Crew limeibuka mshindi na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja taslim na kreti moja ya bia ya Serengeti,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2012.

    Pichani majaji wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 wakijadiliana jambo wakati wa mchuano mkali wa shindano hilo lililokutanisha makundi manne,ambayo ni Tp Jackson,New Kings,B-Boy Dance pamoja na kundi la Contigious Crew.Kulia ni Jaji Msami kutoka THT na shoto ni Mtangazaji kutoka Clouds TV,Issa Kwisa


    Sehemu ya washabiki wa Serengeti Dance la Fiesta 2012 wakivutiwa zaidi na shindano hilo lilipokuwa likiendelea ukumbini humo.
    Kila kundi lilionesha umahiri wake wa kucheza,huku kwa aliyeonekana kufanya vyema shangwe na miluzi ilitawala kila kona.

    Palikuwa hapatoshi jioni ya leo ndani ya Club ya Mawingu wakati wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012 likifanyika,ambapo kila kundi lilionesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma kwa staili ya kipekee kabisa.Pichani mcheza shoo wa kundi la B-Boy Dance akionesha umahiri wake wa kucheza.

    Vijana mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kwenye shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012,ambapo mshindi alifanikiwa kuibuka na kitita cha shilingi milioni moja na kreti moja la bia mshindi wa pili aliibuka na kreti la bia ya serengeti,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo kwa mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI FIESTA SUPER NYOTA ILIVYOFANA M BEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top