Luke Campbell ameing'arisha England katika ndondi, baada ya kushinda Medali ya Dhahabu katika uzito wa bantam kwenye ukumbi wa ExCeL Centre.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Jiji la Hull amempiga rafiki yake na mpinzani wake mkubwa kutoka, Ireland, John Joe Nevin, kwa pointi 14-11
Golden Boy: Luke Campbell
Kichapo: Luke Campbell (kushoto) akimchapa John Joe Nevin
Furaha na maumivu: Campbell akishangilia, huku Nevin akilia
Kichapo kitakatifu: Campbell akidondoka sakafuni baada ya mkono wa kushoto wa nguvu
Wapinzani: Campbell (kulia) na Nevin wakichapana
WASIFU WA CAMPBELL:
1987: Kuzaliwa Septemba 27 mjini Hull.
2007: Alitwaa taji la ABA England.
2008: Alitetea taji la ABA, alishinda taji la Ulaya Liverpool.
2009: Alishinda Medali ya Shaba michuano ya Ulaya Denmark.
2011: Alishinda Medali ya Fedha michuano ya dunia Azerbaijan. Alifuzu kucheza Olimpiki ya London.
2012: Ameshinda Medali ya Dhahabu uzito wa Bantam Olimpiki ya London 2012, akimpiga John Joe Nevin wa Ireland kwa pointi 14-11 kwenye fainali.


.png)
0 comments:
Post a Comment