KOCHA Neil Warnock amemsajili mshambuliaji 'mtukutu' El Hadji Diouf katika klabu ya Leeds United ya Daraja la Kwanza England.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 wa Senegal, amekubali kujiunga na klabu hiyo ya Elland Road bila kupewa mkataba ili kuipigania kupanda Ligi Kuu.
Hadi sasa, Diouf amecheza mechi 300 katika Ligi Kuu ya England, aliyojiunga nayo akitokea Ufaransa, baada ya kung'ara kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002.
Katika miaka yake tisa England, amechezea klabu za Liverpool, Bolton, Sunderland na Blackburn. Pia amewahi kucheza kwa mkopo Rangers ya Scotland kabla ya kujiunga na Doncaster ya Daraja la Kwanza msimu uliopita.
Diouf, aliyekuwa Mwanasoka Bora wa Afrika mara mbili, ameichezea mechi 23 Doncaster, lakini alishindwa kuinusuru timu hiyo ya Yorkshire kuporomoka kutoka Daraja kutoka la Kwanza hadi la Pili.
Warnock alianza kazi Leeds Februari mwaka huu na anafanya kazi katika mazingira magumu mbele ya Mwenyekiti 'Bakhili' Ken Bates kutoa fungu la usajili wa maana.
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk


.png)
0 comments:
Post a Comment