KLABU ya Tottenham inataka kuwapiga bao wapinzani wao, Arsenal katika kuiwahi saini ya kiungo wa Rennes, Yann M'Vila baada ya klabu yake ya Ufaransa, kuthibitisha wamepata ofa ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.
Yann M'Vila
M'baye Niang
Tottenham pia wana matumaini ya kuwapiga bao Arsenal na AC Milan katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Caen, M'Baye Niang, mwenye umri wa miaka 17, kwa ofa waliyotoa ya pauni Milioni 6.
Na mapigo hayo yanakuja wakati Barcelona inatayarisha ofa ya pauni Milioni 11 kwa ajili ya kiungo Alex Song wiki hii.
Wakati huo huo, Nicklas Bendtner anahusishwa na mpango wa kuhamia AC Milan katika dili la kumbadili na Philippe Mexes.


.png)
0 comments:
Post a Comment