![]() |
Abuu Ubwa |
Na Prince Akbar
BEKI
aliyetupiwa virago katika klabu baada ya msimu uliopita, Abuu Zuberi Ubwa
mwenye umri wa miaka 20, ameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na Shirikisho
la Soka Ureno (FPF) ili acheze soka ya kulipwa huko.
Ofisa Habari
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN
ZUBEIRY leo kwamba, mbali na Ubwa, beki wa kushoto ambaye alishindwa
kung’ara Yanga, kwa misimu miwili ya kuwa na klabu hiyo, Hamisi Thabit Mohamed mwenye
umri wa miaka 19, pia kutoka African Lyon pia ameombewa ITC ya kucheza nchi
hiyo.
Kwa mujibu
wa FPF, wote wawili wanaoombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa (amateur) ili
waweze kujiunga na timu ya Atletico Sport Clube ya Ureno ambayo hata hivyo
haikuelezwa iko daraja gani nchini humo.
Pia FPF
imeombwa kupatiwa hati ya maelezo ya mchezaji (player’s passport) kwa kila
mmoja ikiwemo taarifa za ushiriki wao katika mechi rasmi zinazotambuliwa na TFF
wakiwa katika klabu zao hizo za zamani.
0 comments:
Post a Comment