![]() |
Roandlo enzi zake Man United |
Tetesi za Jumapili magazeti Ulaya
SIR ALEX FERGUSON AITAKA BODI IMREJESHE MAN UNITED RONALDO
Sir Alex Ferguson ameitaka bodi ya Manchester United kumrejesha winga wake wa zamani, Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 27, ambaye amesema hana furaha Real Madrid.
Wakati huo huo Ronaldo na Real Madrid wanajiandaa kutoa taarifa ya pamoja kumaliza utata kuhusu mustakabali wa Mreno huyo.
Spartak Moscow iko tayari kuijaribu Arsenal kumnunua mshambuliaji wao, Theo Walcott, mwenye umri wa miaka 23, kwa kuweka dau katika dirisha dogo, Januari mwakani.
Winga wa Manchester United, Nani, mwenye umri wa miaka 25, anataka kuvunja mkataba wake Old Trafford na kuondoka kama mchezaji huru.
Rais wa Lyon, Jean-Michel Aulas amedokeza atajaribu kumsajili kiungo wa Chelsea, Florent Malouda, mwenye umri wa miaka 32, katika dirisha dogo Januari.
Swansea inajiandaa kumsajili beki Mholanzi, Dwight Tiendalli, mwenye umri wa miaka 26, ambaye ametemwa na FC Twente mwishoni mwa msimu uliopita, ili azibe pengo la majeruhi, Neil Taylor.
Liverpool itaunda Kamati ya Ufundi, baada ya kushindwa kusajili mshambuliaji katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili England.
Taarifa kwamba Arsenal ilitaka kumsajili dakika za lala salama katika dirisha la usajili, kiungo wa Anderlecht, Lucas Biglia, mwenye umri wa miaka 25, zilikwama kutokana na ofa ndogo.
ROONEY: HUGO ALITAKA KUNISTAAFISHA SOKA KABISA
Wayne Rooney amesema kwamba rafu aliyochezewa na mshambuliaji wa Fulham, Hugo Rodallega ilitaka kumstaafisha kabisa soka na tayari Chama cha Wachezaji wa Kulipwa kimeingilia sakata hilo.
Kiungo wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain mwenye umri wa miaka 19, atapumzishwa na kocha wa England, Roy Hodgson baada ya kutolewa kipindi cha pili katika mechi ya Ijumaa, timu hiyo ikishinda 5-0 dhidi ya Moldova.
Hodgson anaamini nyota wa England, Tom Cleverley, mwenye umri wa miaka 23, anaweza kucheza kwa kiwango cha nyota wa Hispania, Cesc Fabregas.
Bodi ya Ligi Kuu England, imegoma kuzungumzia sakata la wachezaji kupeana mikono kabla ya mechi, licha beki wa Chelsea, John Terry na Anton Ferdinand wa QPR timu zao kuwa zinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu, mwishoni mwa wiki ijayo.
Peter Crouch, mwenye umri wa miaka 31, akiwa pamoja na mshambuliaji mpya wa Stoke, Michael Owen, mwenye umri wa miaka 32, watatengeneza pacha la hatari, ambalo litawasaidia wawili hao wote kurejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England.
ROONEY YUKO PEACE NA RONALDO
Wayne Rooney amesema hajawahi kuwa na bifu na Cristiano Ronaldo - licha ya mchezaji mwenzake huyo wa zamani wa Manchester United, kumchongea akalimwa kadi nyekundu kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia, mwaka 2006, England ikitolewa na Ureno.
Mchezaji mpya wa Kispnayola wa QPR, Esteban Granero, mwenye umri wa miaka 25, ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Real Madrid mwezi uliopita, ataungana vema wachezaji wenzake wa timu yake hiyo mpya.
0 comments:
Post a Comment