• HABARI MPYA

    Friday, September 07, 2012

    MAUGO KUWANIA TAJI LA WBO NA MUIRAN SEPTEMBA 28

    Maugo

    BONDIA Mada Maugo, anatarajiwa kupanda ulingoni kwenye ukumbi wa Triple A mjini Arusha Septemba 28, mwaka huu kuzipiga na Gavad Zohrenvad wa Iran, kuwania ubingwa wa WBO uzito wa Middle.
    Maugo ameiambia BIN ZUBEIRY kwa sasa yupo kwenye maandalizi makali kwenye pambano hilo na anawaahidi mashabiki wake atalibakisha taji hilo nchini. Hilo litakuwa pambano la kwanza kwa Maugo, tangu apigwe kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya sita na Francis Cheka Aprili 4, mwaka huu.             
    Aidha, hilo litakuwa pambano la 24 kwa Maugo, tangu aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007, akianza na ushindi wa pointi dhidi ya Hussein Chiwa Mei 12, mwaka huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAUGO KUWANIA TAJI LA WBO NA MUIRAN SEPTEMBA 28 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top