Zakaria Hans Pope
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope (kushoto) akimkabidhi mchango wa dola 1,000 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Said Kilumbanga kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa Stars, Alfonce Modest. Modest kwa nyakati tofauti aliwahi kuzichezea timu za Simba, Mtibwa Sugar, Pamba, pamoja na Mlandege ya Zanzibar. Picha kwa hisani ya Habari Mseto Blog.
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ametoa msaada wa dola za
Kimarekani 1,000 (zaidi ya Sh milioni 1.5) kwa beki wa zamani wa kimataifa wa
Tanzania, Alphonce Modest Pambamotosapi, anayesumbuliwa na maradhi ya ganzi.
Modest,
aliyewahi kuchezea Pamba ya Mwanza, Simba, Yanga za Dar es Salaam, Mlandege ya
Zanzibar na Mtibwa Sugar ya Morogoro, yuko Dar es Salaam akiendelea na matatibu
chini ya usimamizi wa gazeti la Championi kwa kushirikiana na Redio ya Magic
FM.
Mtangazaji
wa Magic FM, Said Kilumanga ambaye ni mmoja wa waratibu wa zoezi hilo alisema
tayari Hans Poppe ameshakabidhi fedha hizo, ili kumsaidia beki huyo wa kushoto,
aliyempokea Kenneth Mkapa katika nafasi hiyo timu ya taifa.
“Tunamshukuru
sana Hans Poppe kwa moyo wa kujitolea, wengine pia wajitokeze kumsaidia kwa
kuwa amepungukiwa kama Sh 600,000 tu ili kukamilisha matibabu yake,” alisema
Kilumanga.
Mkurugenzi
wa Msama Promotion, Alex Msama ndiye alikuwa mdau wa kwanza kumchangia Modest
na kuomba wengine wajitokeze kumsaidia beki huyo mahiri wa zamani.
Baadhi ya
wanamichezo wamekuwa wakiendelea kumchangia Modest ili kuhakikisha anapata
matibabu baada ya maradhi hayo kumuandama kwa zaidi ya miaka minne sasa.
(Wanaotaka kumsaidia Modest, wanaweza kupiga
namba 0718 427426 na 0718 427426 kufikisha
misaada yao).
0 comments:
Post a Comment