![]() |
11 walioanza leo |
![]() |
Mrisho Ngassa akiwatoka mabeki wa Sofapaka |
![]() |
Mwinyi Kazimoto akijiandaa kutia krosi |
![]() |
George Owino akimdhibiti Salim Kinje |
![]() |
Haruna Moshi kulia akizungumza na George Owino wakati Akuffo ameumia anapatiwa huduma ya kwanza kabla ya kutolewa |
![]() |
Edward Chiristopher akitafuta mbinu za kumtoka Edgar Ochieng |
![]() |
Edward Chirstopher Edward akimtoka Edgar Ochieng |
Na Mahmoud Zubeiry
SIMBA imeshindwa
kuwafurahisha mashabiki wake jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada
ya kufungwa mabao 3-0 na Sofapaka ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa
kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Jumanne ijayo kwenye
Uwanja huo huo.
Hadi
mapumziko, Sofapaka walikuwa kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji wa
zamani wa Yanga, John Barasa kwa penalti dakika ya 19, akiupeleka mpira kulia
na Juma Kaseja akichupa kushoto upande wa kushoto.
Penalti hiyo
ilitolewa baada ya Komabil Keita kuunawa mpira kwenye eneo la hatari wakati
akiwa katika jitihada za kuokoa hatari langoni mwake.
Mshambuliaji
Danniel Akuffo alitolewa nje dakika ya 40 baada ya kuumia na nafasi yake
kuchukuliwa na Abdallah Juma.
Kipindi cha
pili, Sofapaka walirudi na moto tena na kufanikiwa bao la pili dakika ya 55
mfungaji Barasa tena kabla ya Joseph Nyaga kufunga la tatu dakika ya 66.
Kwa nini
Simba wamefungwa? Walizidiwa uwezo na Sofapaka, ambao walicheza kwa kuelewana
zaidi tangu mwanzo wa mchezo.
Simba SC; Juma Kaseja (1), Shomary Kapombe (15),
Amir Maftah (17)/Paul Ngalema, Paschal Ochieng (5), Komabil Keita (4)/Juma Nyosso,
Mwinyi Kazimoto (14), Salim Kinje/Ramadhani Chombo (12)/, Haruna Moshi (3)/Kiggi
Makassy, Edward Christopher (19)/Nassor Masoud, Daniel Akuffo (13)/Abdallah
Juma na Mrisho Ngassa (16).
Kocha; Profesa Milovan Cirkovick (Serbia)
Sofapaka FC; Duncan Ochieng (39), Anthony Kimani
(11), James Situma (14), Edgar Ochieng (5), George Owino (26), Collins Okoth
(45), Osborne Monday (2)/Thomas Wanyama, Danson Kago (13)/Hashimu Mukwana, Joseph
Nyangit (30), Humphrey Mieno (20)/Robert Binja na John Baraza (19).
Kocha; David Ouma (Kenya)
0 comments:
Post a Comment