![]() |
Akuffo katika mechi ya jana |
Na Mahmoud Zubeiry
HALI ya
mshambuliaji wa Simba SC, Daniel Akuffo ni njema na leo anaweza kuendeleza na
mazoezi na wenzake kwenye Uwanja wa Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam.
Akuffo aliumia
jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Sofapaka ya Kenya, ambao Simba SC
walifungwa kwa mabao 3-0.
Daktari wa
Simba SC, Cossmas Kapinga ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, Akuffo alipata
mshituko mkubwa kwa kuchezewa rafu mbaya ghafla kiasi cha ulimi kugeuka na
kupoteza fahamu, lakini baada ya jitihada za haraka, alipona.
“Jitihada za
haraka za kumpatia tiba makini ya huduma ya kwanza zilisaidia, yuko sawasawa na
hana tatizo lolote, alipoteza fahamu, lakini tulipofanikiwa kuurejesha ulimi
katika hali ya kawaida, ilikuwa mwisho wa tatizo,”alisema Kapinga.
Daktari huyo
wa mabingwa wa Tanzania Bara, alisema kwamba klabu hiyo haina majeruhi zaidi na
wachezaji wanaokosekana kwa sasa ni washambuliaji Mzambia Felix Sunzu ambaye
kwenye mazishi ya dada yake na Emmanuel Okwi ambaye yupo na timu ya taifa ya
kwao, Uganda.
Simba jana
ilishindwa kuwafurahisha mashabiki wake Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya
kufungwa mabao 3-0 na Sofapaka ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa
na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Jumanne ijayo kwenye Uwanja huo huo.
Hadi
mapumziko, Sofapaka walikuwa kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji wa
zamani wa Yanga, John Barasa kwa penalti dakika ya 19, akiupeleka mpira kulia
na Juma Kaseja akichupa kushoto upande wa kushoto.
Penalti hiyo
ilitolewa baada ya Komabil Keita kuunawa mpira kwenye eneo la hatari wakati
akiwa katika jitihada za kuokoa hatari langoni mwake.
Kipindi cha
pili, Sofapaka walirudi na moto tena na kufanikiwa bao la pili dakika ya 55
mfungaji Barasa tena kabla ya Joseph Nyaga kufunga la tatu dakika ya 66.
Mechi ya
jana ilikuwa ya kwanza kwa Akuffo tangu ajiunge na Simba anashindwq kuifungia
bao timu yake hiyo mpya na hiyo unaweza kusema kwa sababu alicheza dakika 40 tu
kabla ya kuumia.
Awali,
Akuffo aliifungia Simba katika kila mechi, kwenye tatu za kirafiki ilizocheza
ikiwa kambini Arusha, dhidi ya Mathare United, (2-1), JKT Oljoro (2-1) na Sony
Sugar (1-1).
Simba
inajiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam dhidi ya Azam FC, ambayo kihistoria hiyo itakuwa mechi ya tano ya
Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili kukutanisha timu nje ya wapinzani wa
jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa
ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na
kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado
inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager,
ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi
hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga
tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa
Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao 2-0.
MABINGWA WA
MECHI ZA NGAO YA JAMII:
Mwaka Mshindi Matokeo
2001 Yanga 2-1 Simba
2010 Yanga 0-0 Simba (3-1penalti)
2011 Simba 2-0 Yanga
0 comments:
Post a Comment