![]() |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk |
Na Ally Mohamed,
Zanzibar
CHAMA cha
soka Zanzibar (ZFA) kimemuandika barua nzito Waziri wa Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk ya kutaka ufafanuzi wa kutosha juu ya hatua
yake ya kuamua kumrejesha kazini Katibu Mkuu aliyesimamishwa, Kassim Haji
Salum.
Katika barua
hiyo iliyoandikwa Septemba 8, 2012 ambayo nakala yake tunayo, ikisainiwa na
Kaimu Rais wa ZFA, Al-haj Haji Ameir, na nakala yake kutumwa kwa Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa
la Michezo la Zanzibar (BMZ), Katibu Mtendaji Baraza la Michezo Zanzibar, Makamu
Rais wa ZFA Unguja, Makamu Rais wa ZFA Pemba na Kaimu Katibu Mkuu wa ZFA
kisiwani Pemba.
ZFA Taifa
kupitia kwa Mwanasheria wake, Abdallah Juma wamemtaka Waziri huyo amsaidie
Katibu huyo kujibu hoja alizosimamishiwa badala ya kuonekana kumkingia kifua.
Katika barua
hiyo imesema suala la kumsimamisha Katibu huyo halikuwa adhabu lakini pia
kumtaka ajieleze si adhabu bali ni fursa sahihi si ya ki-Katiba tu lakini pia ni haki yake ya kibinadamu kwa mujibu wa
sharia ya nchi (natural justice and right to be heard) na wamefanya hivyo kwa
nia ya kujenga hadhi ya afisi ya Waziri huyo na ya ZFA.
Itakumbukwa
kuwa chama cha soka visiwani Zanibar (ZFA) chini ya kikao halali cha kamati
Tendaji kikiongozwa na Rais wa chama hicho, Aman Ibrahim Makungu, kilichokutana
tarehe mwezi uliopita kilitoa maamuzi ya Kumsimamisha Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Haji Salum, huku ikitoa hoja nane
ambazo alitakiwa kuzijibu.
Baadhi ya
hoja hizo ni Kotokuwa na uwezo wa kutumia mitandao, kutoa matamshi ya
kukidhalilisha chama hicho pamoja na kutoa siri za vikao halali vya chama
hicho.
0 comments:
Post a Comment