Tetesi za J'tano magazeti Ulaya
LIVERPOOL KUMSAJILI DEL PIERO
Kuna tetesi kwamba Liverpool inajipanga kufanya usajili wa kushitukiza wa mshambuliaji wa zamani wa Juventus, Alessandro Del Piero, mwenye umri wa miaka 37.
Klabu ya Ligi Kuu Australia, A-League, Sydney FC pia imeripotiwa kutangaza kumsajili mshindi huyo wa Kombe la Dunia.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers alitaka kubadilishana wachezaji, kiungo Jordan Henderson, winga Stewart Downing au beki wa kushoto, Jose Enrique ili kumpata mshambuliaji wa Fulham, Clint Dempsey, ambaye alitaka kwenda Tottenham.
Arsenal inafahamika imempa ofa Andrei Arshavin kuondoka kama mchezaji huru, kwa matumaini kwamba, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 atapata klabu mpya kabla ya dirisha la usajili la Urusi halijafungwa kesho, huku Dynamo Moscow wakiwa mstari wa mbele kuiwania saini yake.
Tottenham Hotspur na Porto zilifikia makubaliano juu ya Joao Moutinho katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili England, lakini upande wa tatu wa wadau wa mchesaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ndio unadaiwa kukwamisha dili hilo.
Newcastle itajaribu tena kumsaini winga Tom Ince, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Blackpool Januari mwakani, baada ya dau lao la awali la pauni Milioni 4 kupigwa chini.
Lyon imeitaka Chelsea kutaja bei ya kumuuza winga wake, Florent Malouda, mwenye umri wa miaka 32, ambaye kwa sasa mambo yake hayamuendei vizuri darajani.
ROONEY ATOA KITABU KIPYA, AMZUNGUMZIA FERGUSON
Katika kitabu chake kipya, mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kutemwa na kocha Sir Alex Ferguson lilikuwa somo kubwa kwake. (Daily Mirror)
Mshambuliaji Sergio Aguero 'amemtibua' kocha wake Roberto Mancini kwa kuamua mwenyewe kwenda kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na Argentina, wakati kwa sasa hayuko fiti hata kuitumikia klabu yake, Manchester City.
Mshambuliaji Lukas Podolski, mwenye umri wa miaka 27, anaamini Arsenal wanaweza kuwa washindaji wa taji kama wataendelea na staili yao ya Jumapili, walipoifunga Liverpool.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Arsenal, Peter Hill-Wood amesema The Gunners hawawezi kushindana na Chelsea na Manchester City katika soko la usajili.
Mashabiki wa Liverpool wa kikundi cha Spirit of Shankly, wamemtaka, Mmiliki MMarekani wa klabu hiyo, Fenway Sports Group kuteua Mtendaji Mkuu mkazi wa Liverpool.
MO FARAH AOMBA KAZI YA UKOCHA ARSENAL
Mshindi wa Medali mbili za Dhahabu za Olimpiki, Mo Farah ameitaka klabu yake kipenzi, Arsenal kumuajiri yeye kama kocha wao wa fitness atakapostaafu kukimbia Riadha.
0 comments:
Post a Comment