TIMU
ya taifa ya vijana wa umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys, imeondoka leo
asubuhi kwenda mkoani Mbeya kuendelea na maandalizi ya kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za vijana Afrika zitazofanyika nchini Morocco mwakani.
Timu
hiyo imepangiwa kupambana na Misri katika hatua inayofuata, pambano hilo
linatarajia kufanyika Oktoba mwaka huu. Serengeti ilipata tiketi ya kumenyana
na Misri, baada ya Kenya kujitoa kwenye michuano hii.
Serengeti
imekwenda Mbeya kwa mwaliko wa Chama cha Soka Mbeya Mjini (MUFA), ambacho, kitaihudumia
kwa malazi, chakula na huduma nyingine ndogondogo na itacheza mechi kadhaa za
majaribio ikiwemo dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons.
0 comments:
Post a Comment