![]() |
Simba na Azam zitafungua pazi la Ligi Kuu Jumanne ijayo kwa mechi ya Ngao ya Jamii |
Na Prince AKbar
MKATABA wa
udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo itadhaminiwa tena Vodacom
utasainiwa Jumanne (Septemba 11 mwaka huu) kwenye ofisi za kampuni hiyo jijini
Dar es Salaam.
Ofisa Habari
wa Shiriksiho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo, ameiambia BIN
ZUBEIRY leo kwamba taarifa rasmi juu ya muda wa kusaini na pande
zitakazoshuhudia hafla hiyo itatolewa hivi karibuni.
Msimu mpya wa
Ligi Kuu, 2012/2013 utaanza Septemba 15, mwaka huu kwa timu zote 14 kujitupa
kwenye viwanja tofauti.
Mechi za
ufunguzi zitakuwa kati ya Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam), Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro), Tanzania Prisons
vs Yanga (Sokoine, Mbeya), Mgambo JKT vs Coastal Union (Mkwakwani, Tanga), JKT
Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Kagera Sugar vs Azam
(Kaitaba, Bukoba) na Toto Africans vs Oljoro JKT (Kirumba, Mwanza).
Mzunguko wa
kwanza (first round) utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye mzunguko
huo mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi hiyo
itamalizika Mei 18 mwakani kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu Shooting
(Kirumba), Mgambo JKT vs African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar
(Azam Complex), Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Sokoine), Simba vs Yanga
(Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Azam (Sheikh Amri Abeid Kaluta) na Polisi
Morogoro vs Coastal Union (Jamhuri).
Endapo Simba
na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa
Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.
Wakati huo
huo: Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi rasmi wa Ligi
Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 kati ya bingwa mtetezi Simba na makamu
bingwa Azam itachezwa Septemba 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment