Cesc Fabregas ameelezea kuchanganyikiwa kwake juu ya namna anavyotumika kwa sasa Barcelona.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania, ambaye ameelezea kuchanganyikiwa kwake na kuchezeshwa sehemu tu tu mchezo, alitolewa dakika ya 63 katika ushindi mwembamba wa Barca dhidi ya Valencia Jumapili.
Licha ya kuanza kwenye mechi zote tatu za La Liga msimu huu, Fabregas anabaki asiye na furaha katika klabu iliyomuibua kisoka na kumkuza kabla ya kuuzwa Arsenal, na kurejea Nou Camp msimu uliopita kwa dau la pauni Milioni 30 baada ya miaka nane ya kuishi London.
Cesc Fabregas akionyesha sura yake isiyo na furaha
Hivi karibuni mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, naye aligoma kushangilia mabao yake dhidi ya Granada kutokana na kutofurahia maisha Santiago Bernabeu
Machungu ya Cristiano Ronaldo hayafichiki Real Madrid
"Kila mmoja anapenda kucheza dakika zote za msimu. Nimekuwa nikisema wakati wote nachezea timu bora duniani, lakini nimekuja hapa kushindana, kujifunza na kufurahia, siyo kuumiza kichwa changu.
"Kocha anajua uwezo wangu. Lakini katika nafasi zote tatu ninazoweza kucheza, nashindana na wachezaji watatu bora duniani. Nafurahi kuwa sehemu ya timu hii, lakini kocha akiniambia natakiwa kuondoka, nitaondoka.
"Lakini sitampa wepesi wa kufanya hivyo, kwa namna yoyote. nitaendelea, kuangalia mbele hadi mambo yabadilike. nimekuja hapa kufanya kazi kwa ufanisi,"alisema Fabregas.
Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2198316/Cesc-Fabregas-complains-life-Barcelona.html#ixzz25agRanUy
0 comments:
Post a Comment