![]() |
Dk Sufiani Juma kulia kabisa akimtoa kiungo Haruna Niyonzima kwenye vurugu. Ameondolewa. |
Na Prince Akbar
KLABU ya
Yanga imefanya marekebisho tena katika benchi lake la Ufundi, kwa kumuondoa Daktari,
Sufiani Juma ambaye nafasi yake inachukuliwa na Dk Nassor Matuzya.
Hayo yanakuwa
mabadiliko ya pili katika benchi la Ufundi la Yanga ndani ya miezi miwili,
kwani awali alienguliwa kocha wa makipa, Mfaume Athumani Samatta ambaye nafasi
yake ilichukuliwa na Mkenya, Razack Ssiwa.
![]() |
Nassor Matuzya. Amechukua nafasi |
Kabla ya
hapo, Septemba mwaka jana, Yanga ilimuengua Kocha wake Mkuu, Mbelgiji Tom
Saintfiet na nafasi yake kupewa Mholanzi, Ernie Brandts.
Yanga SC
iliyorejea wiki Jumapili kutoka Uturuki kwenye kambi ya wiki mbili mjini Antalya,
kesho itashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na Black Leopard ya Afrika
Kusini katika mchezo wa kirafiki.
Black
Leopard inayoshika nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini yenye timu 16,
imewasili leo ikiwa na msafara wa watu 42 na kufikia katika hoteli ya White
Sands, Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Yanga leo
asubuhi imeendelea iliyoanza juzi tangu irejee Uturuki katika Uwanja wa Mabatini,
Kijitonyama tayari kwa mechi ya kesho.