Simba SC jana imefungwa 1-0 na timu ya taifa ya soka ya Oman chini ya umri wa miaka 23 katika mchezo wake wa kwanza wa kirafiki katika ziara yake ya mafunzo nchini Oman. Simba ipo huko tangu wiki iliyopita ikiwa imeweka kambi mjini Muscat na itaendelea kujifua huko hadi mwishoni mwa mwezi. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu' |