• HABARI MPYA

    Thursday, January 17, 2013

    SUPERSPORT TV KURUSHA LIVE MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU BARA


    Na Prince Akbar
    MZUNGUKO wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa na maombi ya televisheni ya SuperSport kuonyesha mechi za Super Week kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
    Raundi tano za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo wakati nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super Week.
    Wakati huo huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya kuanza itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SUPERSPORT TV KURUSHA LIVE MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top