TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 18 ya Chelsea imejitengenezea mazingira ya kutinga fainali ya Kombe la FA la vijana England, baada ya jana kuichapa mabao 2-0 Liverpool .
Chelsea yenye Mtanzania, Adam Nditi kikosini, ilipata mabao yake kupitia kwa Alex Kiwomya, mpwa wa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Chris,aliyefunga katika dakika za 86 na 90 na sasa timu hizo zitarudiana Uwanja Stamford Bridge Ijumaa ijayo.
Mkali: Alex Kiwomya akishangilia mabao yake aliyoifungia Chelsea dhidi ya Liverpool jana