KLABU ya Bayern Munich imemuweka kwenye orodha ya wachezaji inayowataka, beki wa Arsenal, Laurent Koscielny tena wale iliyowapa kipaumbele wakati kocha Pep Guardiola akijiandaa kuanza kazi kwa mabingwa hao wa Ujerumani.
Klabu hiyo ya Bundesliga inatarajia kumpotgeza beki wake wa kati mkongwe, Mbelgiji, Daniel van Buyten na inataka kusajili mchezaji atakayeziba pengo hilo na atayeendana na staili ya kocha mpoya.
Koscielny alikuwa pia akiwaniwa na Barcelona wakati wa msimu wa mwisho wa Guardiola Hispania na tangu wakati huo ameendelea kuimarisha kiwango chake, tokea awasili London miaka mitatu iliyopita.
Mpambanaji: Laurent Koscielny (kulia) alicheza vizuri dhidi ya Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa
Anayetakiwa: Laurent Koscielny (kushoto) anatakiwa na Bayern Munich
Mtu wa kazi: Koscielny amekuwa akiimarika kiuwezo tangu ajiunge na Arsenal
Beki wa Borussia Dortmund, Mats Hummels pia yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa Bayern, ingawa dili lolote baina ya klabu hizo linaonekana kuwa gumu, hususan wakiendelea kumgombea mshambuliaji Robert Lewandowski.
Koscielny mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akimuweka benchi Nahodha wa klabu hiyo, Thomas Vermaelen karibu msimu wote wa 2013, na licha ya kuandamwa na matatizo ya kuumia umia msimu huu, kwa sasa ni tegemeo la Arsene Wenger katika safu ya ulinzi.
Jicho la bao: Koscielny aliifungia Arsenal bao la pili ilipomenyana na Bayern katika 16 Bora Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Allianz, lakini ilitolewa
Ajaye: Pep Guardiola ataanza kazi Bayern Munich msimu ujao
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye amiechezea mechi tisa timu yake ya taifa tangu mwaka 2011, alisaini mkataba mpya msimu uliopita na akizungumzia mustakabali wake hivi karibuni, alisema; "Bado nina mkataba wa miaka minne baada ya Juni. Najisikia vizuri ndani ya klabu- wana imani na mimi. Nina furaha London, familia yangu pia. Sifikirii kuondoka,".