• HABARI MPYA

    Tuesday, April 09, 2013

    AZAM FC YAWAREJESHA KUNDINI NYONI, AGGREY NA WENZAO WALIOTUHUMIWA NAO KUHUJUMU TIMU




    Erasto Nyoni
    Na Prince Akbar
    KLABU ya Azam FC, imewarejesha kundini wachezaji wake wanne, kipa Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Erasto Nyoni, Aggrey Morris na Said Mourad iliyowasimamisha tangu Novemba mwaka jana kwa tuhuma za kuihujumu timu hiyo katika mechi ya mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC.
    Katika mechi hiyo, Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. 
    Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idirsa ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba, baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) dhidi ya wachezaji hao na kubaini hawakuhusika, klabu imewarudisha kundini.
    “Azam FC inatoa taarifa rasmi kuwa TAKUKURU haijawakuta na hatia ya rushwa wachezaji; Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Erasto Nyoni, Aggrey Morris na Said Mourad,”.
    “Hivyo wachezaji hao wanakaribishwa rasmi kurudi kikosini Azam FC kwa ajili ya kujiunga na mazoezi na wachezaji wenzao,”alisema.
    Pamoja na kusimamishwa, Nyoni na Morris waliendelea kuitwa Taifa Stars na kuendelea kufanya vizuri, licha ya kutocheza mechi za ushindani.
    Dida na Mourad, wao walikuwa wakifanya mazoezi tu kwenye maskani zao na kucheza mechi za ‘ndondo’ ili kujiweka fiti wakisubiria hatima zao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM FC YAWAREJESHA KUNDINI NYONI, AGGREY NA WENZAO WALIOTUHUMIWA NAO KUHUJUMU TIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top