UKALI wake wa kufunga mabao ulikuwa chachu nzuri ya mbio za Manchester United, kuelekea kwenye taji la ubingwa wa Ligi Kuu England, kiasi cha wengi kumpa nafasi ya kuwa Mchezaji Bora wa msimu.



Taji la Ligi Kuu dhahiri bado liko kwenye mwelekeo wa kutua Old Trafford, licha ya jana kufungwa na wapinzani wao, Manchester City, lakini bado wana nafasi, tena kubwa ya kubeba ubingwa.
Mabao ambayo yaliifanya United iwaache mbali wengine sasa yamekauka kwa Robin Van Persie, na anaanza kuelekea kuvaa viatu vile vile ambavyo vilipoteza makali ya Fernando Torres tangu atue Chelsea akitokea Liverpool.
Nenda chini katazame video ya mabao ya Van Persie msimu huu
Siku zimebadilika: Robin Van Persie amepoteza makali ya kufunga kwa sasa, baada ya mwanzo mzuri United
TAREHE ZA KUTOLEWA TUZO HIZO
PFA: Mchezaji Bora wa Mwaka- Jumapili, Aprili 28
FWA: Mchezaji Bora wa Mwaka- Alhamisi, Mei 9
Ukame wa mabao haujaisha kama ilivyokuwa kwa Torres kati ya Oktoba 2011 na Machi 2012, alishondwa kufunga bao hata moja ndani ya saa 25 na dakika 41.
Van Persie naye sasa amemaliza saa 11 na dakika 24 uwanjani bila kufunga.
Kutoka na hali hiyo, kuna shaka kama mshambuliaji huyo wa Man United aliyenunuliwa kwa pauni Milioni 24 msimu huu kutoka Arsenal, atapigiwa kura za kutosha kubeba tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA au FWA.
Takwimu za Robin Van Persie msimu huu hadi sasa
Mwanzo mzuri: Van Persie was an instant hit at United as his goals fired them to the Premier League summit
VIDEO Angalia mabao ya Van Persie msimu huu Man United
Shakani: Van Persie alikuwa mshindani anayeongoza katika kinyang'anyiro cha tuzo zote PFA (juu) na FWA chini


.png)