• HABARI MPYA

    Sunday, April 07, 2013

    AZAM NA BARRACK ZAINGIZA MILIONI 44

    Kipre Tchetche wa Azam FC kulia akimtoka beki wa Barack katika mchezo wa jana

    Na Boniface Wambura
    MECHI ya marudiano ya Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania na Barrack Young Controllers II ya Liberia iliyochezwa jana imeingiza Sh. 44,229,000.
    Fedha hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 17,128 waliokata tiketi.
    Viingilio vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A. Kiingilio cha sh. 2,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 15,212.
    Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 5,798,025, asilimia 10 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Sh. 3,865,350 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 28,990,500.
    Mechi iliyopita ya raundi ya Kwanza ya mashindano hayo kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini iliyochezwa kwenye uwanja huo huo Februari 16 mwaka huu iliingiza sh. 34,046,000 kwa viingilio hivyo hivyo huku ikishuhudiwa na watazamaji 13,431.
    Wakati huo huo: TFF imewapongeza waandishi watatu wa habari za michezo kwa kushinda Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) inayotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
     Waandishi hao walioshinda katika kategori ya michezo na utamaduni ni Abdul Mohammed wa The African kwa upande wa magazeti na Abdallah Majura wa redio ABM kwa upande wa redio.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM NA BARRACK ZAINGIZA MILIONI 44 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top