KOCHA Jose Mourinho ameitaka Chelsea kuthibitisha kurejea kwake Stamford Bridge au kujiweka hatarini kumkosa.
Kocha huyo wa Real Madrid anatarajiwa kumpokea majukumu Rafa Benitez mwishoni mwa msimu hiyo ikiwa mara ya pili kwake kufanya kazi Ligi Kuu England.
Lakini Manchester City, Paris Saint-Germain na AC Milan pia zimeripotiwa kumsubiri mkali huyo wa mataji.
Muda unakimbia: Jose Mourinho amejiandaa kurejea Chelsea mwishoni mwa msimu
"Jose anataka kurudi Chelsea. Ni mahali anapotaka kuwa," chanzo kimeiambia The Sun.
"Kila wakati mashabiki wa Chelsea wanaimba jina lake na hiyo inamfanya atake kurejea hata zaidi.
"Atasaini kwa dau lile analopata Real, pamoja na kwamba ana uhakika wa kupata zaidi sehemu nyingine — kama City au PSG.
Mtaa rahisi: Real Madrid itamenyana na Levante usiku wa leo bao wapo nyuma ya Barcelona
"Jose anaweza pia kubaki Madrid, lakini yuko wazi juu ya wapi anapotaka kwenda — sasa ipo juu ya Roman Abramovich ikiwa anataka hivyo.'
Mourinho ameshinda mataji sita na Chelsea ndani ya misimu mitatu, lakini hakuweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa.
Anatarajia kufanya hivyo Uwanja wa Wembley, Mei 25 akiwa na Real Madrid ambayo ina matumaini ya kuingia Nusu Fainali baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Galatasaray wiki iliyopita.
Safari inanukia: Rafa Benitez anatarajiwa kuachia ngazi mwishoni mwa msimu
Benitez hajawahi kukubalika kwa imani za Chelsea, baada ya kuchukua mikoba ya Roberto Di Matteo, aliyetupiwa virago.
Mspanyola huyo ameweka bayana ataachia ngazi mwishoni mwa msimu, lakini atakuwa bado hajatwaa mataji ya Europa League na Kombe la FA.


.png)