Na Mahmoud Zubeiry
HIVI karibuni, Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage pamoja na kusema ataitisha Mkutano Mkuu wa mwaka Julai mwaka huu, pia alisema amekubali kujiuzulu kwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na si Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Zacharia Hans Poppe, aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili.
Rage, alisema ataongoza mwenyewe kampeni za kuhakikisha Hans Poppe anabatilisha uamuzi wake wa kujiuzulu na kuendelea kuitumikia Simba SC. Je, nini msimamo wa Hans Poppe juu ya hili? Fuatilia mahojiano haya baia ya BIN ZUBEIRY na Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
![]() |
| Hans Poppe; Siriui hadi Rage akae na wabaya wake wamalizane amani irudi |
BIN ZUBEIRY: Habari za leo kiongozi
HANS POPPE: Nzuri tu, habari na wewe
BIN ZUBEIRY: Salama, Hivi mlizungumza na Rage kuhusu suala la wewe kubatilisha uamuzi wako wa kujiuzulu?
HANS POPPE: Hapana, bado
BIN ZUBEIRY: Nani anakwamisha mazungumzo kati yenu?
HANS POPPE: Nafasi tu, mimi nimetingwa sana, tangu Pasaka sijatulia Dar es Salaam, hadi nitakapotulia
BIN ZUBEIRY: Wewe ndiye unakwamisha kwa hivyo…lakini kwa kuwa somo unalijua, mtazamo wako ukoje?
HANS POPPE: Nimewashauri wakae kwanza, warejeshe amani, vinginevyo ni kazi bure
BIN ZUBEIRY: Labda wanaamini wewe ukirudi, utasaidia kurejesha amani, unaonaje?
HANS POPPE: Sitarudi hadi kwanza (Rage) azungumze na wanaompinga
BIN ZUBEIRY: Kama msimamo wa Rage uko tofauti na wazo lako, nini mustakabali wa klabu hapa?
HANS POPPE: Lazima wakubali kukutana kwa maslahi ya klabu
BIN ZUBEIRY: Hakuna njia nyingine ya kuinusuru klabu dhidi ya misimamo ya Mwenyekiti?
HANS POPPE: Hakuna
BIN ZUBEIRY: Wana Simba wana imani na wewe na wanakutegemea, kushikilia msimamo wako kwa upande mwingine huoni kama unawaangusha?
HANS POPPE: Siwezi kusaidia kama hakuna amani, kwa hivyo nikiwakutanisha wakaelewana, hakutakuwa na taabu. Shida ni Rage na mdomo wake.
BIN ZUBEIRY: Namini wewe ni Simba damu…
HANS POPPE: Haswaa
BIN ZUBEIRY: Unajisikiaje timu yako inafanya vibaya, kocha hajapata mishahara miezi miwili, klabu inakabiliwa na madeni lukuki, wachezaji hawana ari…vurugu tupu…
HANS POPPE: Inasikitisha na wengi wananipigia, lakini hiyo ndio faida ya ugomvi
BIN ZUBEIRY: Mtakuwa tayari kuvumilia hadi Rage amalize muda wake madarakani?
HANS POPPE: Mimi sina upande, lazima atambue kama hatazungumza nao, hali haitabadilika, kwa hivyo yeye ameshika dhamana ya Simba SC
BIN ZUBEIRY: Lakini unashindwaje kummudu Rage na ni rafiki yako sana, ambaye mnashirikiana hadi katika mambo binafsi?
HANS POPPE: Amekubali kukutana, tatizo utekelezaji
BIN ZUBEIRY: Alikupa ahadi hiyo wewe?
HANS POPPE: Ndiyo, nilimshauri hivyo na akakubali. Inatosha bwana, naingia kwenye mkutano sasa.
BIN ZUBEIRY: Asante kiongozi, kazi njema.
HANS POPPE: Asante nawe na karibu tena.



.png)