KLABU ya Barcelona inajiandaa kubomoa benki kumsajili beki na Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany mwishoni mwa msimu— huku kocha Roberto Mancini amesema anataka kutumia fedha nyingi kusajili ili kupambana na Manchester United.
Mancini amedokeza anataka kutumia zaidi ya Pauni Milioni 100 ili kuwatia presha United na kujiweka sawa katika kampeni za Ligi ya Mabingwa.
Analengwa: Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany anatakiwa na vigogo wa Hispania, Barcelona
Lakini habari kwamba Kompany, mwenye umri wa miaka 26, anaweza kuhamia Nou Camp inaweza kuvuruga hesabu zake.
Nyota huyo wa Ubelgiji alisaini mkataba wa miaka sita na klabu hiyo ya Ligi Kuu England mwaka jana, lakini haiwezi kuzuia uwezekano wa kuhamia Barcelona.
Timu hiyo ya Hispania inataka beki wa kati wa kiwango cha juu azibe pengo la Nahodha wake, majeruhi Carles Puyol, mwenye umri wa miaka 34.
Akiwa ameichezea Hispania mechi 100, Puyol yuko nje msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mwezi uliopita.
Barcelona iko tayari kutoa Pauni Milioni 40 au zaidi na tayari ilionyesha nia ya kumsajili Kompany wakati Pep Guardiola akiwa bado kazini.


.png)